Wednesday, June 26, 2013

ZOEZI LA USAMBAZAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO LIANGALIWE UPYA.


SERKALI imeshauriwa kujipanga na kuimarisha upya zoezi zima la usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa wananchi kwa muda muafaka ili yaweze kusaidia kuongeza tija katika kuongeza mavuno ya nafaka mbalimbali hali itakayosaidia taifa kupunguza tatizo la chakula nchini

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa kilimo na mifugo wa kijiji cha Kitete kata ya kitete wilayani kilosa mkoani Morogoro Jacob Mloka,ambapo alisema kuwa wakulima wengi nchini wamekuwa wakishindwa kupata mazao bora na kwa wingi kwa muda muafaka kutokana na kucheleweshwa kwa ruzuku za pembejeo za kilimo.

 Alisema kuwa ruzuku za pembejeo za kilimo zimekuwa zikichelewa kuwafikia wakulima hasa wa vijijini hivyo kuwasababishia kuvuna mazao machache tofauti na kipindi cha awali amabapo wakulima walikuwa wanavuna mazao kwa kiwango kikubwa ambacho kinawasaidia kuondokana na janga la njaa kutokana na kutumia mbolea na mbegu bora.

Mloka aliswema kuwa kijiji cha kitete kinawakulima wengi wanaolima mazao ya mahindi na mpunga,wengi hawajui kutumia kilimo cha kisasa hivyo kuwalazimu kulima mazoea bila kufuata sheria ya kilimo sambamba na kutotambua mbinu za kubadilisha mazao katika mashamba yao ili kuboresha rutuba katika ardhi wanayotumia katika kilimo.

Alisema kuwa ruzuku za pembejeo za kilimo katika msimu wa kilimo uliopita zilichelewa kuwafikia wakulima hivyo kulazimika kupanda bila kutumia mbolea ambayo ilisababisha mazao kushindwa kukua kwa kipindi muafaka hali iliyosababisha wakulima sehemu mbalimbali nchini kushindwa kuvuna kwa kiwango cha juu hivyo kuifanya nchi kukumbwa na upungufu wa chakula..

Alibainisha kuwa wakulima wa kijiji cha kitete walipewa ruzuku ya kilimo kipindi ambacho tayari walikuwab wamepanda mazao hivyo kusababisha mazao hayo kushindwa kumea vizuri na kupata mavuno bora kutokana na kucheleweshwa kwa ruzuku za kilimo ambayo imekuwa kerp kwa kipindi cha muda mrefu.

Aliiomba wizara ya kilimo kuboresha utaratibu wa utoaji wa ruzuku za pembejeo hasa katika maeneo ya vijijini kwani wakulima wengi wapo maeneo ya vijijini lakini wamekuwa hawasaidiwi katika kuboresha kilimo sambamba na ucheleshwaji wa utoaji wa pembejeo za ruzuku 



Hata hivyo alisema kuwa serikali inatakiwa kujipanga na kuthibiti mawakala wasio na sifa amboa wanaharibu zoezi zima la usambazaji wa pembeje,kuwataka wataalamu wa kilimo kujikita zaidi katika maeneo ya vjjijini..

No comments:

Post a Comment