Thursday, June 27, 2013
KITUO CHA AMANI CENTRE CHAKABILIWA NA UKOSEFU WA FEDHA
Warembo wa Kumsaka Miss Reds Kanda ya Mahariki wakikabidhi vifaa kwa watoto walemavu katika kituo cha Amani Centre mjini Morogoro
KITUO cha Amani Centre kinajihusisha na kulea watoto wenye ulemavu wa aina tofauti kinakabilia na changamoto ya mbalimbali zikiwemo ukosefu wa fedha za kuendeshea huduma kituoni hapo
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa kituo hicho,Baetus Sewando katika hafla fupi liyofanyika kitiuo hapo ya kukabidhiwa msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa washiriki wa redds miss kanda ya mashariki
Sewando alisema kuwa kituo hicho sasa kinajiendesha chenyewe kutokana na miradi yake na kupata msaada kutoka kwa watu ndani ya mkoa wa morogoro baada ya kukosa wafadhili na walikuwepo kusitisha huduma katika kituo hicho
Alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili ni ukosefu wa chakula,mavazi,na ukosefu wa elimu kwa wazazi na walezi watoto wenye ulemavu ya kuwaficha watoto na kuona kuwa ni jambo la aibu katika jamii jambo ambalo halina tija kutokana na watoto hao wana haki sawa kama wenigne wasio na ulemavu
Kwa upande wake Mratibu wa shindano la Miss Reds Kanda ya Mashariki,Alex Nikitas alisema kuwa wametambua nafasi waliyonayo katika jamii,na jamii nyingi za watanzania wamekuwa na tabia ya kutenga watoto wenye ulemavu hivyo kutumia muda walio nao kuwahudumia
Warembo wakikabidhi msaada wa mafuta
Alex alisema kuwa watoto wenye ulemavu wanahitaji huduma nyingi sana hasa kwa upande wa malezi na chakula na waliojitolea kuwapatia huduma wanatakiwa kuwaunga mkono kwa njia mbalimbali ili watoto waweze kupatiwamalezi bora kama watotot weningine walio majumbani
Mratibu huyo alitaja vitu vilivyotolewa ni mchele,sabuni,mafuta na juice,pia aliwataka wadau wengine wa maendeleo pamoja na serikali kuangalia kituo hicho kwani kinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo kwa pamoja kuwalea watoto hao ambao wanahitaji huduma kama wengine
Shindano la kumsaka miss reds kanda ya Mashariki linatarijiwa kufanyika tarehe 29 june katika ukumbi wa Nashera mjini Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment