SHIRIKA lisilo la Kiserikali Morogoro Environmental
Conservation (Moeco) limeunga mkono kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya
kuwataka watanzania kujihusisha na ufugaji wa nyuki kwa kutundika mizinga 60
kwa lengo la kujikwamua kiuchumu na kuchangia pato la Taifa
Zoezi
hilo lilifanyika jana katika Ofisi za shirika lisilo la kiserikali
la Moeco lenye ofisi zake Kata ya Saba Saba
katika kuazimisha siku ya utundikaji mizinga ya nyuki
duniani,kama njia moja wapo ya uamasishaji ufugaji wa nyuki .
Mratibu
wa mradi wa nyuki unaoshirikisha taasisi za Moeco,Sua na Water Loo
foundation ,Jackson Msaliwa alisema kuwa maazimisho
ya siku hiyo ya utundikaji nyuki ni
njia moja wapo ya uamasishaji wananchi kutambua
ufugaji wa nyuki ndio njia mbadala ya kumkwamua mtanzania
kiuchumi .
Msaliwa
alisema kuwa shughuli za ufugaji nyuki , zimekuwa chachu
kubwa ya maendeleo ya kasi kwa wanafanyabiashara
wa zao la nyuki nchini ukilinganisha na biashara
nyingine .
Alisema
kuwa tangu mradi huo kuanza katika vijiji
vya mkundi , Wami , Dakawa , Njovu,Madudu,Kitete, Mfulu ,Lungu
wami sokoine , wananchi wa maeneo
hayo ambao waliamua kujishughulisha moja
kwa moja na ufugaji wa nyuki wameonekana
kujikwamua kiuchumi ukilinganisha na shughuli zao za
awali .
Kwa
upande wake Katibu tarafa wa manispaa ya Morogoro ,Sulpicius
Pakalapakala , akifungua maadhimisho hayo alisema
kuwa serikali inatambua mchangao mkubwa wa
asasi zisizo za kiserikali, hivyo hakuna sababu ya
kutounga mkono jitihada za masharikika hayo .
Alisema
kuwa serikali itaendelea kuayaunga mkono mashirika yote
yenye nia nzuri ya kuleta mabadiliko ya
kiuchumi nchini na sio mashirika yenye nia ya kupoteza amani
ya taifa .
Mwanachama
wa asasi ya Moeco ,Dk Ally Fungo ameiomba serikali
kuendelea kutoa ushirikiano na mashirika yasiyo ya
kiserikali , hususani masharika yanayojihusisha na utunzaji wa
mazingira kwani yanajitahidi sana katika kutunza mazingira na kutoa elimu kwa
jamii .
Hata
hivyo alisema kuwa taifa limekuwa na uharibifu mkubwa
mazingira hali ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha
ukosefu wa mvua , ikiwa pamoja na mabadiliko ya
taibia nchi .
No comments:
Post a Comment