WAKULIMA
wa miwa katika bonde la Ruhembe wilayani Kilosa wamelalamika kuwa hawanufaiki na
kilimo hicho kutokana na utata unaojitokeza katika kuhakiki ubora wa sukari
inayopatikana kutoka kwenye miwa yao wakati wanapoipeleka kwa mnunuzi ambaye ni
kiwanda cha sukari cha Ilovo.
Wakizungumza
katika mkutano wa mkuu wa mwaka wa chama
cha wakulima wa miwa katika bonde la Ruembe wilayani Kilosa,wakulima hao
walisema kwamba kukosekana kwa usimamizi
thabiti kutoka upande wa wakulima wakati wa kuhakiki ubora wa sukari toka
kwenye miwa yao kumekuwa kukisababisha kupata mapunjo ya gharama halisi ya miwa
yao kutoka kwa mnunuzi huyo.
Wakulima
hao walisema wanachokitaka wao ni kupatikana kwa uwakilishi wa wakulima
wakati wa kupima ubora wa sukari yao pale inapofika kiwandani ili waweze kujua
halisi ya kiwango cha sukari yao.
Aidha
wakulima hao walilalamika pia kupunjwa wingi wa miwa wanayopeleka kiwandani
jambo linalowafanya kurudi nyuma kiuchumi sambamba na kuvuniw miwa kwa
kuchelewa jambo wanaloamini linatokana na kukosekana kwa mwakilishi wa wakulima
wakati wa upimaji kiwandani hapo.
“Wakati
wa tunavuniwa miwa sisi tunaona ni mingi na yenye ubora lakini cha kushangaza
ni pale tu unapofika kiwandani tunapewa vocha ndogo ambazo hazilingani na ubora
wa muwa ,na wakati mwingine utakuwa mtu analipwa kiasi kidogo kama shilingi
150,000 malipo haya hayakidhi hata gharama ya shamba uliotumia,”alisema Musa
Mpunuge mkulima wa miwa
Wakulima
hao walisema kuwa pamoja na kupunjwa wingi na ubola wa miwa lakini bado
wanakabiliwa na changamoto kuunguzwa moto kwa mashamba yao mara kwa mara jambo
linalolalamikia kuwa linaweza kupunguza ubora huo.
Joyce
Kisaka mkulima wa miwa katika bonde hilo la Ruembe alisema kuwa changamoto
nyingine ni kulipwa malipo madogo kutokana na umbali wa mashamba jambo
linalowakatisha tamaa wakulima wengi wa bonde hilo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama hicho Msabaha Nyembe aliwataka wanachama
kutotumika vibaya na baadhi ya wenzao
kwa kutaka kuvuruga chama kwa maslahi yao binafsi, ikiwemo wanaoanza kampeni za
kutaka uongozi ndani ya chama hicho.
Aidha
mwenyekiti huyo alisema chama hicho kimeendelea kuimarika siku hadi siku, na kwamba kimeweza kununua
vitendea kazi kusadia kilimo na juvunaji wa miwa ikiwa ni pamoja na kata pila
na mitambo ya kupakia na kushusha miwa yenye thamani ya zaidi ya shilingi 600
milion.
No comments:
Post a Comment