Baadhi ya Waandishi wa habari wa Mkoani Pwani wameadhimisha siku ya ukimwi dunia kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Buloma,Pichandege wilayani kibaha,ambapo kati ya watoto hao,watano wazazi wao walikufa kutokana na ugonjwa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kituoni hapo Mkurugenzi wa kituo hicho Mama Anna Kiando amesema watoto hao walipimwa mara kadhaa na bahati nzuri hawakukutwa na maambukizi ya VVU .
Akikabidhi misaada hiyo Mwamvua Mwinyi mwandishi,ambae pia ni makamu Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoani Pwani,amesema wametoa mchele,unga,sukari,sabuni za kufulia,maji katoni kumi,mafuta ya kupikia,juice na Biscuit vyote vikiwa na gharama ya Tsh Laki Tano.
Aidha kwa niaba ya waandishi mkoani humo,amemshukuru Mbunge wa jimbo la kibaha Mjini,Silvestry Koka,Kampuni ya maji ya Lulu,Lebul Kontena na Kobil Chalinze kwa ushirikiano wao kufanikisha misaada hiyo.
Kiando ameshukuru kupata misaada hiyo na ameaomba wadau kujitokeza kusaidia watoto hao ili waweze kukidhi mahitaji yao sanjali na masuala ya kielimu kwani yeye pekee inakuwa ngumu kutimiza masuala yote muhimu.
No comments:
Post a Comment