Meneja wa NMB kanda ya Mashariki Bw Gabriel Ole Loibanguti
akimkabidhi msaada wa madawati Mwl mkuu wa shule ya msingi
ya Mvumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro .
Kilosa .
Jumla ya
watoto 216 katika shule ya msingi ya Mvumi
wilayani Kilosa mkoani Morogoro wameondolewa adha ya kukalia
mikeka na mawe wakiwa darasani kufuatia benki ya
NMB mkoani Morogoro kutoa msaada wa madawati 85 na meza tano
vitu vyote vikiwa na tahamni ya shilingi mil 5.
Akiongea na
waandishi wa habari jana katika hafla hiyo fupi
,afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa Bw Ayoub
Kambi kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo alisema
kuwa benki hiyo imekuwa msaada mkubwa katika kutatua
kero mbalimbali zinzoikabili sekta ya elimu .
Bw
kambi alisema kuwa wilaya ya Kilosa imekuwa
na changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu
lakini taasisi hiyo ya fedha ya NMB
imekuwa mkombozi mkubwa katika kuzitatua kero
hizo kwa kiasi kikubwa .
“Ni kweli
watoto wengi wanakaa chini madarasani hali ambayo inawafanya
wanashindwa kufanya vizuri kimasomo darasani kutokana na
kusoma katika mazingira mabaya “alisema Bw kambi
Alisema
kuwa ni wazi maombi ya misaada katika
taasisi hiyo yamekuwa mengi kutoka maeneo
mbalimbali ya kanda ya mashariki , lakini wilaya ya
kilosa imekuwa na bahati katika kufanikisha maombi yao
.
Aidha
alisema kuwa kwa kiasi kikubwa benki hiyo
imekuwa ikisaidia kupunguza mzigo wa halmashauri na wazazi
katika kutatua changamoto zilizopo katika
sekta ya elimu .
Alisema
kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia misaada mbalimbali katika shule za msingi na
sekondari hivyo kwa niaba ya wakazi katika wilaya ya
Kilosa na halmashauri yake hana budi kuishukuru NMB .
Aidha
naye meneja wa NMB kanda ya mashariki Bw
Gabriel Ole Loibanguti akizungumza katika hafla hiyo ya
kukabidhi madawati hayo na meza kwa mbele ya
kamati ya wazazi na uongozi wa shule ya
msingi Mvumi aliwataka wazazi kuhakikisha wanaendeleza
watoto kielimu .
Alisema
kuwa benki ya NMB kwa kutambua umuhimu wa
elimu kwa watoto ndio mana imekuwa mstari wa
mbele katika kuchanga shughuli za maendeleo ya
sekta ya elimu na sio kuchangia shughuli za hanasa .
Aidha
katika hatua nyingine Bw Loibanguti aliwataka wazazi
kuacha tabia ya kuchangia zaidi shughuli za
hanasa kama ngoma , unyago , kitchen part na harusi na badala
yake kujenga tabia ya kuwawekea watoto
akiba kwa ajili ya kuwaendeleza kielimu .
Alisema
kuwa NMB inayo huduma ya akaunti ya
watoto maarufu kwa jina na Junior akaunti imekuwa njia
sahihi ya kumfanya mtoto kusoma shule
bila ya kuwa na wasiwasi wa kukatisha masomo kutokana na
uhaba wa pesa .
Aidha
meneja huyo wa kanda ya mashariki wa NMB
aliwataka wazazi shuleni hapo kuhakikisha kila mtoto
anafunguliwa akauti ya Junior ili kumfanya mtoto asome akiwa
huru bila ya wasiwasi .
.
No comments:
Post a Comment