MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero
Frolent Kyombo amewaomba waaandishi wa Habari wanaofanya mradi shirikishi wa
utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji kupitia Klabu ya waandishi wa
Habari Morogoro (MOROPC) kuandika habari sahihi zenye tija ili kuweza
kuirudisha wilaya katika hali ya amani.
Kyombo alitoa mwito huo,katika uzinduzi wa mradi huo uliofadhiliwa na The Foundation
For Civil Society (FCS) na kutakiwa kufanyika katika kata za Hembeti, Dakawa na Mvomero ambapo, alisema
kuwa suala la migogoro ya ardhi limegubikwa na uwanja mpana wa jamii na kwamba
upembuzi yakinifu ufanyike kabla ya kuandika habari husika.
Alisema, ikiwa wanahabari watatumia taarifa wanazokusanya na kupata majibu kwa wahusika kabla ya kuzitoa wataweza kutoa habari zitakazojenga na sio kubomoa Mvomero katika suala zima la migogoro hiyo.
Alisema, suala la migogoro ya wakulima na wafugaji wilayani humo lipo na limeshaanza kufuatiliwa kwa kiasi kikubwa na kwamba kwa ujio wa mradi huo unaohusisha wanahabari anaimani wanaweza kuwapatia suluhisho la kutibu tatizo hilo kufuatia kuwa wafukunyuzi wa mambo.
Aidha alisema, kufuatia mradi huo kuwa na lengo la kuzungumzia masuala ya Amani utasaidia jamii kuweza kuona umuhimu wa uwepo wa Amani na hivyo kufanya migogoro hiyo kupungua au kuisha kabisa.
Awali Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani hapa (MOROPC) Nickson Mkilanya alisema, lengo la mradi huo nikushirikisha jamii katika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji wilayani humo ili kurejesha amani.
Mkilanya alisema, kufuatia kuona migogoro hiyo ikishambulia katika eneo hilo zaidi licha ya kwamba eneo jingine ipo wameamua kuomba ufadhiliwa huo toka FCS na kuweza kuangalia namna ya kurejesha Amani iliyokuwepo awali ambayo sasa imeonekana kutoweka.
Alisema, migogoro hiyo katika wilaya hiyo imeweza kuleta maafa ya binadamu na wanyama na pengine kuleta athari zingine mbalimbali kwa jamii ikiwemo uharibifu wa mazao na mapigano yaliyosababisha majeruhi .

Wialaya ya Mvomero ni miongoni mwa wilaya
zinakumbwa na migogoro ya ardhi mara kwa mara na kusababisha uvunjivu wa
amani,hivyo wananchi kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji zinazoweza
kuwapatia kipat
Mwisho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment