Wednesday, May 7, 2014

SHERIA ZA KULINDA WATOTO ZIHESHIMIWE.



KITUO  cha msaada wa kisheria cha Morogoro Paralegal kimeitka jamii inayolea  watoto wa kambo na wale walioasili watoto kuwalea kwa kuzingatia kanuni na sheria kwa kuwapatia mahitaji muhimu na ya msingi kama watoto wengine

Akizungmza na MHAKITA, Mkurugenzi wa kituo hicho Flora Masoy na walisema  kuwa watoto hao ni sawa na watoto wengine na wanapaswa kulea watoto katika mazingira yanayostahili kwa kupatiwa mahitaji yote

Masoy alisema kuwa watoto wa kambo au wa kuasiliwa wanastahili heshima na kuthaminiwa kama ilivyo kwa watoto wengine kwa kupatiwa haki za msingi ikiwemo kupendwa, elimu, kusikilizwa, kuabudu, mavazi  na kuishi

Kwa upande wake Mwanasheria wa Kituo Msaada wa Sheria Amani Mwaipaja alisema kuwa malezi ya watoto yapo kwa mujibu wa sheria zinazolinda watoto na hivyo ni wajibu wa kila mwanajamii kuona umuhimu wa taratibu za sheria zilizowekwa

Mwaipaja alisem kuwa watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili mara kwa mara na walezi wao wa kuwazaa ama wa kuwalea jambo mbalo linamjenga motto kuishi katika mazingira magumu ndani ya familia bila kujali haki za watoto

Alisem kuwa imefika mahali kila jamii iwe mstari wa mbele katika kuktetea haki za watoto ambao wnategemew kw taifa lijalo na pale wanapoona mtoto anafanyiwa kitendo kibaya wawe wa kwanza kukemea na kutoa taarifa katika vyombo vya sheri mhusika aweze kupewa chukuliwa hatua stahiki

Mwisho.

No comments:

Post a Comment