Morogoro.
Mamlaka ya maji safi na
maji taka mkoani Morogoro (Moruwasa) imetangaza hali
ya ukame uliokithiri katika vyanzo vya maji tegemezi
vinavyotegemewa kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi
kwa wakazi mkoani Morogoro .
Rai hiyo imetolewa
hapo jana na mkurugenzi mtendaji wa Moruwasa , Bw
John Mtaita wakati akiongea na timu ya wanahabari
iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia kwa kina kero
mbalimbali za wananchi mkoani Morogoro .
Bw Mtaita alisema
kuwa hali hiyo ya ukame uliokithiri
imetokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo
chanzo chake kikubwa ni uharibifu wa mazingira unaokithiri
katika maeneo mabalimbali hususani mkoani Morogoro .
Alisema kuwa tatizo
la ukame wa maji limekuwa kubwa katika
limekuwa kubwa sana ukilinganisha na miaka ya
nyuma , ambapo kila ifikiapo kipindi cha kiangazi maji
upungua kwa asilimia arubaini tu , lakini kwa mwaka
huu maji yamepungua kwa kiasi cha zaidi ya
asilimia 60.
“Ningependa niwaambie wananchi
hali hii itaendelea kuleta shida katika maeneo yote ya
Manispaa mpaka hapo mvua zitakapoanza kunywesha “
alisema Bw Mtaita .
Hata hivyo mkurugenzi
huyo alidai , wananchi wanatakiwa kujua kuwa mahitaji ya watu
yameongezeka kwa kiasi kutokana na kutanuka kwa mji
ukilinganisha na siku za nyuma wakati mitambo ya maji
ikijengwa ..
Alidai kuwa hali
hiyo itapungua mara tu baada ya kukamilika
kwa mradi wa amji wa MCC ambao utazalisha maji mita za
ujazo zaidi ya 36,000 kwa siku .
Alisema kuwa mradi
huo wa MCIT ambao upo chini ya mradi mama wa MCC
unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka 2013 , hata
hivyo amedai kuwa pamoja na mradi huo kukamilika
lakini bado wananchi wanahitaji kupewa elimu juu
ya umuhimu wa kutunza mazingira hususani vyanzo
vya maji .
Timu hiyo ya
waandishi wa habari mkoani Morogoro ambayo ilitembelea
katika baadhi ya vyanzo vya maji vya Mafiga
,Mindu,Maturi na Mambogo na kushuhudia hali hiyo .
Kufuatia hali
hiyo ya ukame mkoani Morogoro kwa sasa wananchi
wamekuwa wakinunua ndoo ya maji ya lita ishirini kwa
kiasi cha shilingi mia nne mtaani
.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka Bw John Mtaita akielezea hali ya ukame wa maji katika vyanzo vya maji ndani ya manispaa ya Morogoro , kama inavyojieleza picha ya Bwawa la Mindu lilivyokauka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na uharibifu wa mazingira..
kcaption |
Add cap |
No comments:
Post a Comment