Tuesday, November 10, 2015

SERIKALI YASHAURIWA KUBORESHA MFUMO WA USIMAMIZI WA MADINI

SERIKALI  ya  awamu ya tano imeshauriwa kuhakikisha inaweka mfumo mzuri zaidi wa kusimimamia sekta  ya madini  hapa nchini  ili kuweza kupiga hatua zaidi kimaendeleo na kukuza uchumi  wake kama ilivyo nchi ya Afrika ya  kusini .

Ushauri huo umetolewa jana na Mtaalamu  wa madini ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MTL Consulting ambayo inajishughulisha na  ushauri wa sekta ya madini nchini John Tindyebwa wakati akitoa  mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya ulewa juu ya  masuala ya madini na sheria yake ya mwaka 2010 kifungu namba 4.

Tindyebwa alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa Waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro  yana  lengo la  kuwapa ulewa juu ya   mradi mpya wa  Kampuni ya Kibaran  resources Limited inayochimba madini  ya Kinywe (Graphite) katika machimbo Epanko Mahenge yaliyopo  wilayani Ulanga mkoa Morogoro.

Alisema kuwa  ni vyema serikali ya awamu ya tano ikahakikisha inaweka mfumo mzuri zaidi utakaosaidia kuinua sekta ya madini  kama zilivyo nchi nyingine mfano nchi ya nchi  Afrika kusini ambapo imeonekana kupata mafanikio makubwa kutokana  na kuweka mipango  na mikakati mbalimbali katika  suala zima katika sekta ya madini.

‘’Tunaishauri serikali ya awamu ya tano ikaweka mfumo mzuri zaidi katika usimamizi wa sekta ya madini  ili watanzania waweze kunufaika na rasilimali ya madini na kukuza uchumi ‘’alisema .
.
Alitolea mfano mji wa Johannesburg uliopo nchini Afrika ya Kusini  kipindi cha mwaka 1890 ulikuwa masikini lakini baada ya kipindi kifupi kugundulika kuwa  madini na nchi  kuweza kuweka mfumo mzuri wa usimamizi wa madini yake  nchi imeweza kukua kiuchumi na hata kujengekea na kuwa miongoni mwa miji mikubwa duniani ambao umekuwa kwa kasi kutokana na sekta ya madini.


Pia alibainisha kuwa nchi ya  Tanzania sio nchi masikini kwani imejaliwa kuwa na rasimili kubwa ya madini ya aina mbalimbali lakini imeshindwa kuyatumia kutokana na kutokuwepo na mfumo mzuri zaidi wa usimamizi wa rasilimali hiyo.


Kwa upande wao wanahabari wakichangia mada  inayohusu sekta ya madini na uanzishwaji wa migodi  Joseph Malembeka na Nickson Mkilanya  walisema kuna haja ya serikali  kuwatumia wataalamu wa jiolojia katika kubaini maeneo yaliyo na uwezekano wa upatikanaji wa madini ili kuweza kutambulika na kuepuka adha ya kuwahamisha wananchi kiholela.


Hata hivyo waliishauri serikali  kuweka sheria na mikataba ya wazi  kwa wawekezaji itakayosaidia wananchi  kunufaika na sekta ya madini hapa nchini kutokana na mali hizo kupatikana ndani ya ardhi ya Watanzania

Mwishho.


No comments:

Post a Comment