Wednesday, September 30, 2015

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AONGOZA MAZISHI YA CELINA KOMBANI MJINI MOROGORO

Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Mama Salma Kikwete,Spika wa Bunge Anna Makinda wakisoma ratiba ya mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Utumishi Menejementi ya Umma  Celina Kombani katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro

Askari wa Bunge wakiingiza geneza la  mwili wa marehemu Celina Kombani katika uwanja wa jamhuri Mororgoro aliposomewa ibada ya kumuaga kabla ya mazishi yaliyofanyika katika shamba lake Lukobe.

Mwili wa Marehemu,Celina Kombani ukiwa katika uwanja wa jamhuri huku ibada ya maombolezi ikiendelea.

Viongozi wa serikali na Chama cha Mapinduzi wakiaga mwili huo katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro

Spika wa Bunge,Anna Makinda wakipeana pole na Mama Salma Kikwete katika ibada ya kumuaga Mh.Celina Kombani mjini Morogoro.

Baadhi ya waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Utumishi Menejimenti ya Umma Celina Kombani mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment