Monday, September 28, 2015

KAMPUNI YA M-POWER YAFUNGUA OFISI MKOANI MOROGORO.

                                              
Meneja wa Opereshani wa kampuni ya M-Power,Emanuel  Ngandu akitete jambo na viongozi wa serikali za mitaa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya kamapuni katika kata ya Kihonda Magofani.

Wafanyakazi wa Kampuni ya M-Power wakimpokea Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Rajabu Rutengwe katika uzinduzi wa ofosi yao.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Dkt.Rajabu Rutengwe akikata utepe wa uzinduzi wa ofisi ya M-Power,kulia Mkurugenzi wa Usambazaji wa M-Power,Raphael Robert katika Kata ya Kihonda Magorofani

Mkuu wa mkoa wa Morogoro,Dkt.Rajabu Rutengwe akiongea na wananchi na wafanyakazi waliohudhuria hafla ya hiyo.

Viongozi waliohudhuria hafla hiyo wakigonga cheers kwa ishara ya upendo baada ya ufunguzi wa Ofisi ya M-Power mkoani Morogoro.

Wafanyakazi wa Kampuni ya M-Power wakifanya maandazi ya ufunguzi wa ofisi yao iliyopo Kata ya Kihonda Magofani mkoani Morogoro.

Afisa Utumishi wilaya ya Morogoro,Emmanuel Nzunda,akitetea jambo na viongozi wa kampuni ya M-Power kabla ya ufunguzi wa ofisi ya kampuni hiyo iliyopo kata ya kihonda magorafani.


MKUU wa mkoa wa Morogoro Dk Rajabu Rutengwe amewataka wananchi wa mkoani hapo kununua umeme wa nishati ya jua M-Power Tanzania kutokana na huduma zao kupatikana kwa urahisi na kila mtu anaweza kumudu gharama zao.


Dk Rutengwe alisema hayo mjini Morogoro wakati akifungua ofoisi za M-Power tawi la Morogoro zilizopo katika kata ya  Kihonda Magorofani,ambapo alisema huduma ya nishati ya umeme ni muhimu sana hasa jamii wanazoishi hivyo kuwaunga mkono kampuni.

Aliitika kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma hiyo katika maeneo ya pembezoni mwa miji hususani walioko vijijini ambao maisha yao ni duni ili kuondokana  na ununuzi wa mafuta ya taa na mishumaa ambayo imekuwa ikisababisha hasara ikiwamo ya kuungua kwa nyumba na magonjwa ya macho

Alisema ni azma ya serikali kushirikiana na wadau wa maendeleo kama ilivyo kwa M-Power Tanzania katika kuwakwamua wananchi kuondokana na wimbi la utegemezi wa nishati ya umeme moja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa usambazaji wa MPower kwa nchi ya Tanzania na Rwanda,Raphael Robert alisema kampuni yake inatarajia kutoa huduma za bure kwa taasisi za serikali kama Vituo vya Afya,Zahanati pamoja na vituo vya Polisi ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi wake nyakati zote.


Robert alisema mpaka sasa  kwa nchi za Afrika wamefanikiwa  kufikia nchi ya Rwanda, na Tanzania nia yao ni kuwafikia watu wa hali ya chini ambao wamekuwa wakishindwa kupata huduma ya umeme ya wakawaida.

Mwisho

No comments:

Post a Comment