Ponda akiwa chini ya ulinzi wa polisi akipelekwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfadhiwa wa mkoa wa morogoro kujibu mashitaka yaliyokuwa yanamkabili. |
Ponda akitoka mahakamani baada ya kusomewa mashitaka matatu yaliyokuwa yanamkabili na kukana yote,kurudihswa gerezani hadi Augusti 28.kesi itakapoendelea. |
Askari wakiweka ulinzi mkali mara baada ya mahakama kumalizika na wakiwa tayari kumrudisha Ponda katika viwanja vya gofu kupandihswa kwenye hedikopta na kurudishwa Dar es salaam. |
ULINZI mkali uliimarishwa katika maeneo ya manspaa ya Morogoro wakati Katibu wa taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda mkazi wa Dar es salaam jana alipofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu shitaka linalomkabili huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi wakiwa na mbwa baada ya kuwasili kwa herikopta ya jeshi la Polisi katika uwanja wa Gofu mjini Morogoro.
Wakili wa Serikali,Bernard Kongola alikisoma mashitaka matatu dhidi ya Shekhe Ponda Issa Ponda mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Richard Kabate ,alisema mnamo Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Kiwanja cha Ndege manispaa ya Morogoro Ponda Issa Ponda aliwaambia “ndugu waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bwakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali na kama watajitokeza kwenu watu hao na watajitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti,fungeni milango na madirisha ya msikiti yenu na muwapige sana”
Kongola aliimbia mahakama kauli ambayo ilikuwa ikiumiza imani za watu wengine,na kwamba hatua hiyo ni kinyume cha agizo la mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar-es-salaam iliyotolewa na hakimu V. Nongwa tarehe mei 9 mwaka huu ambayo ilimtaka ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani, ambayo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 124 cha mwaka 2002, shitaka ambalo alikana.
Ponda akishuka kwenye gari nje ya makahama. |
Katika shitaka la Pilli,mshitakiwa, Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Kiwanja cha Ndege manispaa ya Morogoro na mkoa wa Morogoro waliwaambia waislam serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua,kuwabaka, na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni waislamu lakini serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa ,mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni wakristu na kusema kuwa maneno ambayo yaliumiza imani za watu wengine ambalo ni kinyume cha kifungu cha sheria 129 cha mwaka 2002shitaka ambalo pia mashtakiwa Ponda Isa Ponda alikana.
Shitaka la tatu ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria mkuu wa serikali Bernard Kongola kuwa mnamo agosto 10 mwaka huu eneo la kiwanja cha ndege manispaa na mkoa wa Morogoro mashitakiwa aliwashawishi waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu uliyotokana na gesi kwa kuwaua,kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni waislamu lakini serikali haifanya hivyo kwa wananchi wa Liliondo walipotaka Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni wakristo”
Wakili upande wa serikali alisema kuwa maneno ambayo yalikuwa yakiumiza imani za watu wengine na kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002, shitaka ambalo pia nalo Shekhe POnda Issa Ponda alikana.
Kwa upande wa utetezi,Ponda alikuwa akitetetewa na wakili Ignas Pungu na Bantalomeo Tarimo,huku upande wa serikali walikuwa wanaongozwa na Benedict Kongola,Gloria Rwakibalila, Asnab Mhando
Shekhe Ponda Issa Ponda aliwasilishwa kwa hedikopta ya jeshi la polisi katika uwanja wa Gofu mjini morogoro akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kupandishwa katika gari maalum ambalo liliongozana na magari mengine matatu ya polisi huku ulinzi ukiwa umeimalishwa katika eneo la mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro wakiwemo askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia ,wa upelelezi usalama wa taifa pamoja na mbwa wa jeshi la polisi wakati shughuli za kazi katika mahamaka hiyo na ofisi za jirani zikiwa zimesimama kwa muda.
Alifikishwa uwanja wa mahakama majira ya saa 5.00 kamili asubuhi magari yalisimama kwa takribani dakika 30 ndipo askari walishuka kwenye gari na kumfungulia mlango kisha kushuka na kuongozwa kwenye mahakama ya wazi ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Morogoro huku umati wa wananchi ukiwa umefurika mahakamani hapo na kushuhudia kilichokuwa kinaendelea
Baada ya Kusomwa kwa mashtaka yote matatu wakili wa serikali aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi umekamilika na kupanga kesi kuanza kusikilizwa septemba 2 mwaka huu ambapo kwa upande wa utetezi uliomba mahakama kupanga kuanza kusikilizwa kwa kesi agosti 26 mwaka huu hali ambayo ilimlazimu hakimu Kabate kuwapa muda wa kujadiliana ambapo walitumia dakika tano kujadiliana na kurejea mahakamani na kupanga kuanza kusikilizwa kesi agosti 28 mwaka huu.
Mawakili wa upande wa utetezi walisema sababu za kuomba terehe hiyo ya kusikilizwa kwa kesi kwa kile walichoeleza kuwa mteja wao bado ni mgonjwa na anahitaji kupatiwa matibabu ya mara kwa mara hivyo anahitaji uangalizi
Hata hivyo mahakama ilipomalizika hali ya ulinzi iliendelea kuimarishwa na kupandishwa kwenye gari maalum alilopanda na kuelekea kwenye uwanja wa Gofu majira ya saa sita mchana na kupandishwa kwenye hedikopta kwa ajili ya kurejeshwa gerezani jijini Dar-es-salaam.
No comments:
Post a Comment