Saturday, July 27, 2013

WAKULIMA 30 WAVAMIZI WAKAMATWA MVOMERO.

SERIKALI Wilayani Mvomero imewakamata wafugaji  wafugaji 30 wavamizi  wakiwa na ng’ombe zaidi ya 5,000 katka opereshani maalumu wa kuwaondoa  wafugaji wavamizi waliongia wilayani humo bila kufuata taratibu na sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka alisema kuwa zoezi hilo ni kuhakikisha wilaya hiyo inabaki na wafugaji wenyeji,  ili kuondoa ukosefu wa chakula unaosababishwa na wafugaji hao kwa kulisha mifugo
mashambani  na wakati mwingine kusababisha migogoro ya ardhi

Mtaka alisema  wafugaji hao wanashikiliwa kwenye kituo kikuu  cha polisi wilayani humo  kilichopo Dakawa huku mifugo yao ikiwa imeachiwa kwa kukosa sehemu ya malisho na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Alisema wakulima wilayani humo wamekuwa wakijitahdi kulima, lakini baadhi ya wamekuwa wakikosa mazao kutokana na wafugaji wavamizi kulisha mifugo, nakwamba wamejipanga kuhakikisha
kunakuwa na mavuno ya kutosha na kuondokana na baa la njaa.

Alisema msako huo ulianza majuma mwili yaliyopita na kwamba unafanywa na uongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo.

Aidha Mtaka alilalamikia  kitendo kinachofanywa na baadhi ya viongozi mwa vyama vya kisiasa  kwa kufanya upotoshaji katika jami kuwa inawahamisha wafugaji hao bila kufuata taratibu maalum zilizowekwa.

Hata hivyo alisema wanaohamishwa ni wageni, na kudai kuwa wenyeji wanaachwa na kwamba msako huo unafanywa kwa kushirikiana na viongozi wa kimila wa wafugaji waliopo ambao wanawafahamu vizuri ili kuondoakan na malalamiko yatakayoweza kutokea.

Mvomero.

No comments:

Post a Comment