Mwakilishi wa Benki ya CRBD,Issa Singano akimkabidhi Salum nakala za pikipiki. |
Makamu Mkuu wa chuo cha Mzumbe Prof.Joseph Kuzilwa akimkabidhi ufunguo wa bajaji mwanafunzi Salum Mnagwe. |
JUMUIYA ya
chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirkiana na Benk ya CRDB imemzawadia mwanfunzi mwenye
ulemavu wa miguu Salum Mnagwe pikipiki ya tairi tatu(bajaji) yenye thamani ya
shilingi mil.6.1 kutokana na mwafunzi huyo kuonyesha jitihada mbalimbali
alipokuwa chuoni hapo.
Akimkabidhi
pikipiki hiyo jana ,Makamu Mkuu wa chuo cha Mzumbe Prof.Joseph Kuzilwa alisema
kuwa mwanafunzi huyo alionyesha jitahada nyingi sanaalipokuwa chuoni hapo has
kuonyesha kwa jamii jinsi gani ya kuwajali watu wenye ulemavu
Prof.Kuzilwa
alisema kuwa kijana salumu muda wote wa miaka mine alipokuwa chuoni hapo
alishirikia katika shughuli mbalilmbali walizokuwa wanafanya wanfunzi wenzake
bila kujali ulemavu wake na kuwa kama mfano kwa walemavu wenigine na jamii
inayomzunguka
Alisema kuwa
jumiya ya mzumbe kwa kushirikiana kwa pamoja wafanykazi na baadhi ya wanafunzi
na benki ya CRDB waliona ni jambo la busara kumtafutia mwanfunzi huyo
aliyehitimu masomo yake pikipiki ambayo itamsaidia katika kutoka sehemu moja
kufanya kazi zake
Kwa upande
wake Mwakilishi wa benki ya CRDB,Issa Singano alisema kuwa wao walipopata
taarifa za kijana salumu walichukua suala hilo na kulifanyia kazi mapema
kutokana na mtindo wa benki hiyo ya kujali sana maslahi ya jamii na wateja wake
kwa jumla
Singano
alimtaka mwanafunzi huyo mhitimu kutumia pikipiki salhiyo katika matumizi
mazuri na kukitunza ili kuweza kudumu na kumsadia kwa kipindi cha muda mrefu
anapokuwa katika shughuli zake za utafutaji wa maisha.
Mwanafunzi
Salum Mnangwe ni mlemvua wa miguu ,amehitimu mafunzo ya taeknolojia ya
habari kwa miaka minne katika chuo kikuu
mzimbe morogoro.
No comments:
Post a Comment