SERIKALIimesema kuwa uandikishaji wa watoto wanaokwenda katika shule za msingi nchini umepanda kwa 95% hali ambayo imetokana na mpango maalum wa serikali wa kutakakila shule nchini kuwa na darasa la elimu ya awali.
Hayoyammebainishwa na Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi ambaye pia ni Mbunge wajimbo la Bagamoyo Docta SHUKURU KAWAMBWA katika kijiji cha Kerege alipokuwaakizungumza na wakazi wa kijiji hicho wakati wa ziara yake ya kukagua kuhimizana kuzungumza na wakazi wa jimblo lake.
Docta KAWAMBWAamesema serikali ilitoa waraka namba 2,ambao ulikuwa ukiwataka maafisa elimu wamikoa nchini kuhakikisha wanatekelezaagizo hilo la serikali la kuanzishwa akwa madarasa ya elimu ya awaali kwa kilashule za msingi ili kutoa fursa kwa watoto wengi kuandikishwa darasa la kwanzawakiwa na na uelewa na ufahamu utakaowasaidia katika elimu yao ya msingi.
Docta KAWAMBWAwizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kwa kuzingatia maendeleo ya elimu nchiniiliamua kutoa waraka namba 2 kwa maafisa elimu wa mikoa nchini ili wawezekuhakikisha wanafuatilia ujenzi wa vyumba vya madarasa ya elimu ya awali kwakila shule nchini na hili limewezekana kwani uandikishaji wa watoto wanaokwendadarasa la kwanza nchini umeongezeka kwa 95%.
Katika hatuanyingine Kawambwa amewataka wenyeviti wa vitongoji wilayani Bagamoyokuhakikisha wanasimamia kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweka hali ya mambo sawa katikamaeneo yao na kuepusha migogoro inayotokea mara kwa mara na kukwamishautekelezaji wa majukumu yao ya kikazi.
Kawambwa amesemahayo kufuatia kukumbana na maswali na kero nyingi ambazo zimekuwa zikiulizwakwake na wakazi wa maeneo mbalimbai na kuongeza kuwa ni jukumu la viongozi haona watendaji wa vijiji na halmashauri kuhakikisha wanafuatilia kero za wananchibadala ya kukaa na kumsubiri Mbunge.
No comments:
Post a Comment