Monday, September 17, 2012

MUME Mkatili Mkazi wa DodomaMakulu Bw. Paulo Enea wa, aliwashambulia kwa Mpini wa kubebea Mkaa au Maji Mkewake Bi Eunice Emmanuel (42) na watoto wake wawili Bw. Maiko Enea (15) na Bi. VersiEnea (14) nusura ya kuua.

Bw. Enea aliwashambulia mkena wanawe Jana Jumapili Septemba16, 2012 saa Moja Usiku, huku mkewe akiwa katapakaadamu kwa kupasuka usoni, akitafuta kituo cha Polisi akiongozana na Bi. Versi aliyekuwahajiwezi na kiwiko chake kikiwa kumegeuka.

Akizungumza na mwandishialiyekwenda Hospitali ya Mkoa kuchunguza hali za majeruhi wa ajali ya Kondoa,Bi. Emmanuel akiwa anachuruzika damu ili hali amembeba mtoto mdogo wa mwakammoja aliamuomba mwandishi amuonesha kituo cha Polisi ambapo, alimweleza kuwawamepigwa na Mchi mumewe Bw. Enea nusura ya kufa.

“Mume wangu ametupiga nawatoto na Mchi nusuru ya kufa, kilichotuokoa na mwanangu Lwange ambalo nilipigana watu wakaja kutusaidia, lakini kama si hivyo mwanagu wa kike Bi, Versiangekuwa wa kwanza kufa, akifuatia kaka yake na mwisho mimi”.alisema Bi.Emmanuel kwa tabu.

Alipoulizwa kisa cha Mumewekuwashambulia na watoto alisema, mwanae alikwenda kwa mama yake mdogo na aliporudialianza baba yake alianza kumshambulia, na kwa kuwa uchungu wa mwana anaujuamzazi, alilazimika kumuokoa mtoto na kipondo kibaya alichokuwa akipata, jambolilimsabishia kupigwa vibaya na mwanae wa kiume.

Mama huyo alisema, baada yakuelemewa alilazimika kupiga Lwange (Ngolo) iliyowaleta watu kuwasaidia, nandipo mtoto wa kiume aliponyoka na kukimbia hadi kituo cha Polisi, akidhanimama na dada yake wamekufa, jambo ambalo mwandishi alipofika polisi walisema nayealikuwa ametoka si muda mrefu.

"Nilimsamehe mara ya kwanza aliponipiga hadi nikatoka jino nikarudi kwa wazazi wangu, laakini kwa sababu tena ni mjamzito, ndugu zanu waliniomba nirudi nikajiuguze kwake nikakubali, lakini pamoja na kurudi balaa ndiyo hii, namfikisha polisi aadhibiwe naye".alilalamika Bi. Emmanuel


Aidha Polisi mmoja wa Kikena wa kiume waliokuwa zamu, walikubali kuwapokea majeruhi hao na kuahidi kuwapaPF-3 wakishapokea maelezo yao, lakini walikata wasipigwe picha mbele yao kwasababu za kiusalama, hasa kutokana na mwandishi kutaka ampige picha mama upandewa kulia wa uso aliopasumka vibaya.

No comments:

Post a Comment