Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Morogoro akiongea na wafanyabiahara wadogo,hawaonekani pichani. |
SERIKALI imewataka wafanyabiashara wadogo
kuacha kufanya biashara kwa mazoea bila kuwa na mawazo ya maendeleo ya baadae
wakati serikali ikijipanga kuhakikisha inawalinda na kuwapatia maeneo muhimu ya
kufanya biashara zao
Kauli hiyo imetolewana Kaimu Katibu Tawala
wa Mkoa wa Morogoro,Noel Kazimoto wakati akifungua semina ya Kuwajengea uwezo
na kuwarasimisha wafanyabiashara wadogo wadogo iliyoandaliwa na Taasisi ya
Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Africa Mashariki na kusini (ESAURP)
Kazimoto alisema mkoa wa morogoro una wimbi
kubwa la vijana ambao hawana ajira rasmi,na kujihusishana vitendo viovu,kukaa
vijiweni na kufanyabiashara haramu kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali na
wengine kukosa mitaji
Aliwataka washiriki wa semina hiyo kuwa
mabalozi katika maeneo wanayotoka ili kuweza kuwabadilisha wafanya biashara
wenzao kuacha kufanya biashara bila kufuata taratibu na pia kufanya biashara
katika maeneo yaliyotengwa na serikali
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa
ESAURP,Prof.Ted Maliyamkono ili wafanyabiashara kusonga mbele lazima
watambulike na serikali kwa kusajiliwa,kulipa kodi na kuweza kuwa na cheti cha
kinatambulika na kuweza kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha ama mifuko
ya jamii
Pro.Maliyamkono alisema wafanyabiashara
wadogo Tanzania wako zaidi ya bilioni 4,na katika utafiti wao waligundua
wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kutotambuliwa na serikali,kufanya
biashara bila kuwa na leseni,huku biashara hizo zikifanyika katika maeneo sio
rasmi.
Nae Meneja wa Mradi,ESAURP,Florentina
Sallah alisema mradi huo unatekelezwa katika mikoa kumi,na lengo nikufikia watu
1500 na kila mkoa wafanyabishara 150 wanapatiwa elimu ya kutunza kumbukumbu ya
biashara,mipango mikakati ya biashara,na jinsi ya kupata huduma katika taasisi
za fedha na mifuko ya kijamii.
Mfanyabiashara Joyce Mhamaka alisema kuwa
wajasiriamali wengi wanakabiliwa na changamoto ya mitaji,kutokuwa na elimu
endelevu ya biashara,kutokuwa na leseni na sehemu rasmi ya kufanya biashara na
kujikuta mara nyingi wanakimbizana na mgambo wa mji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment