WANANCHI wilaya ya Kilosa wameiomba serikali kutenga bajeti maalumu itakayotumika kwaajili ya kutoa elimu ya matumizi bora ya ardhi kwa wananchi hususani wa vijijini ambayo itakayosaidia kuwepo kwa matumizi sahihi ya ardhi na kuepuka na migogogoro ya ardhi inayotokea mara kwa mara
Hayo yalisemwa na Wakazi wa kata ya Malolo Tarafa ya Mikumi Wilayani Kilosa Haruna Idd mwenyekiti wa kijiji cha Malolo na Ally Ramadhani Mkazi wa kijiji walipokuwa wakishiriki mafunzo ya matumizi bora ya ardhi na kutambua dhamani yake yalioandaliwa na asasi ya kiraia ya greenbelt trust fund ya mjini hapa yaliolenga kupunguza migogoro ya ardhi na mipaka wilayani Kilosa na kuongeza uzalishaji kupitia ardhi.
Walisema kuwa mpango huo wa utoaji wa elimu ya matumizi bora ya ardhi unafanywa na taasisi ya greenbelt trust fund kwa kushirikiana na asasi ya the foundation for civil society itawasaidia wananchi kuongeza uelewa juu ya umiliki na matumizi sahihi ya ardhi ambayo awali hawakuwa nayo na kupunguza migogoro amabyo haikuwa lazima kutokea.
Idd alisema kuwa wananchi wa vijijini wilayani humo ikiwemo Malolo hawawezi kuutekeleza mpango huo wa matumizi bora ya ardhi uliopitishwa na serikali kwa haraka kutokana na kukabiliwa na umasikini wa kipato na elimu katika kaya na kutika serikali kuangalia hilo kwa karibu zaidi
“Huu ni mpango wa kitaifa ulioanzishwa na serikali sasa iweje uelekezwe kwa wananchi wa vijijini bila ya kutengewa mafungu “ alihoji Haruna Idd mwenyekiti wa kijiji cha Malolo.
Naye Ally alisema kuwa licha ya serikali kuanzisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao dhima yeke ni kulinda rasilimali ardhi kwa wananchi wa vijiji bado inatakiwa kutambua kundi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na kusahaulika.
Changamoto zinazowakabili wananchi hao ni pamoja na vijiji vyao kutopimwa kisheria, vijiji kutokuwa na wataalamu wa kutosha, elimu duni na umasikini umekuwa ukiwasababisha kukosa fedha na kupima maeneo yao kisheria.
Alliongeza kuwa elimu ya matumizi bora ya ardhi kwa wananchi wa vijijini wilayni Kilosa ndiyo njia pekee itakayowasaidia kumiliki ardhi kihalali na kuacha tama ya kuuza kwa wageni kwa bei ya kutupa kwa kujikimu na kuwaacha wakihangaika kutafuta maeneo ya kendeshas kilimo cha kujikimu.
Wananchi wa vijiji mbalimbali wilayani Kilosa na Kilombero wameanza kunufaidika na elimu ya matumizi bora ya ardhi kwa msaada wa asasi za ya kiraia ya greenbelt trust fund ya mjini hapa na the foundation for civil society ya jijini dar es salaam itakayowasaidia kuongeza uzajilishaji kupitia matumizi bora ya rasilimali ardhi kwa kupunguza migogoro ya mipaka na kuongeza uzalishaji mali kupitia sekta ya kilimo ili kuleta maendeleo katika jamii
No comments:
Post a Comment