Thursday, October 11, 2012

WAKULIMA WASHAURI MGOGORO UTATULIWE HARAKA, KILOSA


MGOGORO wa ardhĂ­ kati ya wakulima na wafugaji wa Kata ya Msowero, wilayani Kilosa, umeanza kutokota tena, kufuatia kifo cha mkulima anayedaiwa kupigwa na wafugaji.

Wakulima katika eneo hilo sasa wanatishia kufanya maandamano makubwa ya kushinikiza mgogoro huo umalizwe haraka.Mkulima huyo anayedaiwa kuuawa ametajwa kuwa ni Shaban Msambaa, na inasemekana alikufa Agosti 14, mwaka huu nyumbani kwake Dumila.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa jana na ndugu zake na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mambegwa, yaliko mashamba na makazi yake ya kudumu, Said Ally, Januari 25 mwaka huu, Msambaa alivamiwa na kupigwa na kundi la wafugaji, wakati akijaribu kuzuia mifugo kula mazao yake.

“Baada ya kupigwa yale maumivu yameendelea mpaka yamemsababishia kifo chake,” alisema mwenyekiti huyo.

Habari zilidai kuwa siku hiyo, Msambaa alivamiwa na kundi la wafugaji wa jamii ya Kimasai wapatao saba na kumjeruhi kichwani kwa kutumia rungu.

Zilisema watu hao pia walimkata kwa sime katika sehemu zingine za mwili na baadaye kutelekezwa shambani akiwa amepoteza fahamu. Baadaye aliokotwa na majirani na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, alikolazwa na kushonwa nyuzi 12 kichwani.

Mwenyekiti wa kijiji hicho alisema afya ya Msambaa iliimarika kiasi na kuruhusiwa kurejea nyumbani, lakini baadaye jeraha la kichwani lilianza kuvuja usaha na kumsababishia maumivu makali na hatimaye kufa.

Mwenyekiti huyo wa kijiji aliueleza ujumbe wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata), uliotembelea kijiji hicho jana kufuatilia utatuzi wa mgogoro huo kwamba licha ya kifo hicho matukio ya wakulima kujeruhiwa na wafugaji yameendelea kuongezeka.

“Tangu tukio la kupigwa, Msambaa mpaka sasa hapa ofisini kwangu yameripotiwa matukio mengine manane ya wakulima kujeruhiwa, mojawapo ni la mwanamke kupigwa na kudhalilishwa kijinsia alisema.hicho walisema wanashindwa kutekeleza ipasavyo shughuli za kimaendeleo ikiwemo kilimo kwa kuhofia kufanyiwa vitendo vibaya na wafugaji kama vile kubakwa.

No comments:

Post a Comment