Monday, October 15, 2012

WAFANYAKAZI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA MAZOEZI

WAFANYAKAZI wa mfuko wa Bima ya afya(NHIF) wameshauriwa   kushiriki michezo kwa ajili ya kuboresha afya hatua itakayowafanya kutekeleza lengo la elimu wanayoitoa kwa wanachama wao juu ya kuzingatia michezo kuboresha afya kwa vitendo badala ya wao kuwa wahubiri pekee.

Ushauri huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa utumishi na utawala wa NHIF Beatus Chijumba wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya netiboli kati ya timu ya NHIF na  polisi Morogoro ambapo Polisi Moro iliifunga NHIF bao 31 -12.

Chijumba alisema NHIF imekuwa ikitoa elimu kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla kuzingatia suala la michezo kwa lengo la kuboresha afya zao kwa kuwa na uzito unaolingana na urefu ili kuepukana na magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari shinikizo la damu na mengine.

Alisema katika kutilia msisitizo suala la michezo NHIF ina sehemu ya mazoezi ya Gym ambpo wafanyakazi wamekuwa wakitumia kufanyia mazoezi na kuimarisha afya zao na wataendelea zaidi kusisitizia michezo.
 
                                                        
Naye  Jane Kijazi mwakilishi wa timu ya NHIF alisema mabao walioyapata kwa upande wao ni ushindi mkubwa  na imedhihirisha kwamba timu hiyo ni nzuri kimichezo kwani timu hiyo ya mpirawa mikono  ya polisi imekuwa ikishiriki mashindano makubwa.

Alisema kufanya vizuri kwa timu hiyo kumeonyesha wazi kwamba wana uwezo wa kushiriki mashindano ya wizara na idara za serikali(SHIMIWI) mwakani.

Naye Adson Kitanda kocha wa timu ya polisi alisema kuwa ushindi wa NHIF ni nzuri kwani timu ya polisi imekuwa ikishiriki mashindano makubwa na kushika nafasi ya tano katika ligi kuu ya mchezo huo pamoja na kushiriki mashindano ya afrika mashariki.

Kitanda pia aliomba uongozi wa NHIF kwa mwakani katika mashindano yakiwamo ya SHIMIWI kuweza kuwasaidia kupata jezi ambazo zitaisaidia timu hiyo kuzivaa.

                                                      

No comments:

Post a Comment