Baadhi ya Wafanyakazi wa Bima ya afya wakimsikiliza Mkurugenzi wa Afya wa SUA kabla ya kukabidhi vifaa walivyotoa katika zahanati ya Mazimbu. |
Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) wakiwa katika picha ya pamoja na wauguzi wa zahanati ya Mazimbu-Morogoro
Mkurugenzi wa Utumishi na utawala wa mfuko wa Bima ya Afya,
Beatus Chijumba akionyesha shuka walizotoa katika zahanati ya
Mazimbu
Mkurugenzi wa Mfuko wa bima ya Afya ya Taifa (NHIF) akimkabidhi Mkurugenzi wa Afya wa Chuo Kiku cha Kilimo (SUA) mashuka na baadhi ya vifaa vya kutoa huduma ya afya |
JAMII imetakiwa
kutumia rasilimali zinazowazunguka kujiunga na mifuko ya bima ya afya badala ya
kuondokana na dhana ya kujiona kwamba ni maskini hivyo hawawezi kujiunga
na mifuko hiyo jambo ambalo linawasababisha kushindwa kupata huduma nzuri
katika vituo vya afya na zahanati pindi wanapopata matatizo.
Afisa habari mwandamizi wa mfuko wa
bima ya afya(NHIF) Luhende Singu alisema hayo wakati wakikabidhi misaada kwa
hospitali ya Mazimbu inayomilikiwa na chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine(SUA)
ambapo wakikabidhi ,shuka 40zenye thamani ya shilingi 280,000 pamoja na
miswaki,sabuni,dawa za mswaki,mataulo madogo,juisi vyote vikiwa na thamani ya
shilingi 500,000.
Singu alisema kuwa jamii nyingi za
kitanzania wamekuwa wakishindwa kujiunga na mifuko ya bima ya afya ikiwemo
mfuko wa afya ya Jamii (CHF) na mfuko wa bima ya afya NHIF kwa kisingizio cha
kujiona kwamba maskini wakati wangeweza kutumia rasilimali walizonazo kupenda
kuzitumia kikamilifu.
“jamii ni vyema ikatambua kuwa suala
la afya ni muhimu kujiwekea akiba kwani mtu anaweza kuumwa na kipindi
hicho akawa hana fedha kabisa za kuweza kujitibia au kutibia familia
lakini akiwa mwanachama wa CHF na familia au mwanachama wa
NHIF anatibiwa kulingana na uwanachama wake hata kama huna
fedha”aliongeza kusema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
utumishi na utawala wa NHIF,Beatus Chijumba alisema kuwa NHIF licha ya
wanachama wake kuchangia huduma lakini wamekuwa wakitoa huduma hizo bure
kwa makundi maalum wakiwemo wazee,watoto yatima wajawazito wanaotoka katika
familia maskini pamoja na familia zao .
Chijumba alisema mpango huo umeanza
tangu mwaka jana na kwamba wananchi katika mikoa ya Lindi naTanga ambako
wameanza nako wamefaidika na huduma hiyo kwa lengo la kusaidia jamii katika
suala zima la huduma ya afya na jamii ya watanzania ituunge mkono katika zoezi
hili kwani lengo ni kuhakikisha huduma nzuri inapatikana kwa wakati muafaka
Alisema wameamua kutoa msaada kwa
hospitali ya Mazimbu kwa kuwa pamoja na kutoa huduma kwa jamii lakini wamebaini
huduma za afya zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
vifaa vya tiba,madawa na mengine hiyo msaada huo utasaidia
katika kuhudumia wagonjwa pindi wanapofika kupata huduma katika zahati hiyo
Mkurugenzi wa huduma za afya katika
chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA),dk Omari Kasuwi mara baada ya kupokea
vifaa hivyo alisema kuwa hospitali hiyo ina dawa za kutosha za kuhudumia
wagonjwa lakini wanakabiliwa na changamoto za kutokuwa na baadhi ya vipimo
hivyo kulazimika kuwapeleka katika hospitali za rufaa kama Muhimbili na
kwingineko kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Dk Kasuwi alisema hospitali hiyo
inapokea wagonjwa kati ya 150 hadi 200 kwa siku wenye matatizo mbalimbali
yakiwemo ya ugonjwa moyo,malaria,kansa na kwamba wanalaza wagonjwa lakini
wamekuwa wakiombwa na jamii kutoa huduma ya chakula hospitalini hapo ambapo kwa
hilo chuo kinajipanga kulifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment