Thursday, October 11, 2012
Chama cha wafanyabiashara,Wenye viwanda na wakulima mkoani Pwani-TCCIA-kinakabiliwa na changamoto ya wafanyabiashara wake kukosa masoko ya kuuzia bidhaa zao hali inayosababisha kushindwa kulipa ada kwa wakati na kusababisha chama hicho kuyumba.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano mkuu wa chama hicho, Mwenyekiti wa Chemba hiyo ya TCCIA Mkoa,Kasa Mlonja amesema ukosefu wa soko la uhakika unapelekea wafanyabiashara hao kushindwa kuuza bidhaa zao kwa uhakika.
Amesema wapo wafanyabiashara wao ambao wamefanikiwa katika soko lakini kati ya hao ni wale waliopata nafasi ya kuuza bidhaa zao nchi jirani na katika maonyesho mbalimbali.
Mlonja amebainisha kuwa mji wa kibaha upo njiani lakini malighafi zimekuwa zikipatikana Jijini Dar es salaam hali inayosababisha kutumia kipato kikubwa katika usafirishaji.
Aidha amesema japo hali ya kimapato haikidhi mahitaji ya wanachama wake lakini haina budi kuwaomba wanachama hao kulipia ada kwa wakati ili chemba hiyo iweze kusimama .
Hata hivyo Mlonja amesema serikali mkoani humo imewahakikishia kuwepo kwa soko la kisasa hivi karibuni ingawa muda wa utekelezaji wa soko hilo haujawekwa wazi.
Akizungumzia suala la hisa amewaomba wanachama hao kijumla kununua hisa za TCCIA Investment Company ili hali kukuza mitaji yao .
Uongozi wa chama hicho unamaliza uongozi wake hivyo wanachama wamewekwa sawa kujipanga tayari kwa uchaguzi utakaofanyika April mwaka 2013.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment