Monday, September 17, 2012
UKATILI WA KIJINSIA UKOMESHWE KWA WAKINAMAMA
JAMII wilayani Bagamoyo imetakiwa kutokomezana kupinga uonevu na ukatili wa kijinsia ili kulinda haki za wakinamama dhidiya ukatili wanaofanyiwa kila siku kwa kinamama na watoto.
Wito huoumetolewa na Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bagamoyo mheshimiwa SaidMkasiwa wakati akifungua mafunzo maalum ya haki za wanawake na jinsia wilayanihumo mafunzo yanayoendeshwa na Mtandao wa maendeleo ya wanawake wilayani humo –BAWODEN-.
Hakimu MKASIWAamesema kuwa jamii wilayani humo imekuwa ikishindwa kutetea na kupinga uonevudhidi ya wanawake na jinsia na hivyo kupelekea kuwapo kwa matukio mengi yakuvunjwa kwa haki na kutokufuatwa kwa sheria kuhusiana na masuala ya wanawake .
Amesema jamiiyetu imekuwa ikishindwa kujua au kwa kuogopa kutokomeza uonevu na ukatili dhidiya wanawake hali ambayo imekuwa ikichochea masuala ya ukatili na unyanyasajidhidi ya wanawake na watoto nakuwataka wanawake hao kuwa mabalozi wazuri kwawenzenu katika kupinga ukatili huo.
Awaliakizungumza katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa BAWODEN bibi NURU MHAMI amesemakuwa mtandao huo ulinzishwa kwa ajili ya kutetea haki na maendeleo ya kinamamawilayani Bagamoyo na kwa ujumla malengo ya mtandao huo yamefanikiwa kwa kiasikikubwa.
Amesema kuwamtandao huo umekuwa ukifanya jitihada za kuhakikisha unawawezesha wanakimamakuingia katika shughuli za uzalishaji mali kwa kujiari wenyewe japo wengi waowamekuwa wakikata tamaa mapema wanapoona shughuli za kujiongezea kipatowanazozifanya hazina mafaniko ya haraka.
Mhami amesemakuwa mafunzo hayo yaliondaliwa na mtandao wake yanashirikisha zaidi ya watu 360,kutoka kata zaZinga,Kiromo,Yombo,Magomeni,Pera,Ubena,Bwilingu na Msoga na yamefadhiliwa nashirika la Foundation For Civil Society.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment