Wednesday, July 3, 2013

SEKONDARI YA MBUYUNI YAPATA COMPYUTA 25.


SHIRIKA lisilo la kiseriklia la tanZED la nchini Ireland limetoa msaada wa kompyuta 25 katika shule ya sekondari ya Mbuyuni iliyopo manispaa ya Morogoro kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kufahamu matumizi kompyuta tangu wakiwa sekondari ili kupambana na changamoto zinazowakabili
  
Makamu mkuu wa shule hiyo ya sekondari Mbuyuni Festo Kayombo alisema kuwa shirika hilo limetoa msaada huo baada ya kuridhishwa na utawala wa shule hiyo na hivyo kuamua kutoa kompyuta hizo ikiwa  ni programu ya shirika hilo kusambaza kompyuta kwa shule za sekondari nchikwa lengo la kuendeleza sekta ya elimu

Kayombo Alisema kuwa shule hiyo baada ya kutapa msaada huo imeanza utaratibu wa kutoa mafunzo ya Kompyuta kwa awamu kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajiwa kumaliza ili wamalizapo wawe na uelewa watakapo endelea na msomo ya juu.

Kayombo alisema pamoja na kupata msaada huo uongozi wa shule utashirikiana na uongozi wa kata ya Mbuyuni kuhakikisha jamii inayozunguka shule hiyo kujifunza kwa utaratibu utakaopangwa  ili na jamii hiyo iweze kunufaika na mradi huo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya mbuyuni  Samueli Msuya akikabidhi msaada huo aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kutumia kompyuta hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo kulingana na walimu wao wanavyowaelekeza 

Aliwataka walimu na uongozi wa shule kusimamia kikamilifu na kuvitunza vifaa hivyo ili kuweza kukaa kwa muda mrefu na kuweza kuwasaidia wanafunzi wanaoingia shuleni hapo kila mwaka kuweza kufaidika pia.

Msuya alisema lengo ni kuhakikisha kila mwanafunzi anaemaliza anafahamu kutumia kompyuta kwa lengo la  kuendana na utandawazi na kuweza kufanya vizuri watakapoendelea na  elimu ya juu kutokana na vyuo vingi wanasoma kwa njia ya tovuti

Shule ambazo mpaka sasa zimeweza kupata msaada wa kompyuta kwa manispaa ya Morogoro ni pamoja na shule ya  Sumaye,SUA, Top stars,Lupanga,Mafiga,Kiwanja cha ndege,Kihonda,Nguzo, na Belnard Benderd.


No comments:

Post a Comment