Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania-OUT-
imetoa msaada wa mashuka kwa wagonjwa wa hospitari ya wa saratani ya Ocean road jijini Dar es salaam ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya
chuo kikuu hicho nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992
. Akikabidhi msaada huo Rais wa Serikali ya wanafunzi wa
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania OUTSO ndugu JOHN MLAGULA amesema msaada huo ni
kutambua mchango na huduma inayotolewa na hospitali ya ocean road katika utoaji
huduma za kiafya kwa wagonjwa wa saratani nchini.
Amesema katika maadhimisho hayo open university students
organisation outso imekabidhi mashuka 110 kwa oungozi wa hospitali ya ocean
road ili kuboresha huduma kwa wagonjwa wanao hudumiwa.
Hatahivyo rais huyo wa
serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu huria ameahidi kuchanga michango kila mwaka
kutenga siku maalumu kwa ajili ya kupeleka msaada wa hali na mali katika
hosopitali hiyo
.Naye muuguzi mkuu wa hospitali ya ocean road ndugu MARY
HAULE ameshukuru kwa msaada huo na kuhimiza watanzania wengi kuchangia kwa
kutafutia ufumbuzi wa mahitaji mbalimbali ya hospitali hiyo inayohudumia
watanzania wengi.
No comments:
Post a Comment