Sunday, August 12, 2012
WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUHAMASISHA SENSA
Morogoro
WAANDISHI wa Habari Mkoani Morogoro wameshauriwa kushirikiana kikamilifu na uongozi wa Mkoa katika kuhamasisha wananchi umuhimu wa kuesabiwa katika zoezi la sensa itakayofanyika kuanzia Agusti 26 mwaka huu ili kuweza kufikia lengo lilokusudiwa na serikali katika kuleta maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera alisema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake na kusema suala la sensa ni la kitaifa hivyo haina budi vyombo vya habari kuzidi kuhabarisha umma kuhusu suala zima la sensa.
Bendera alisema kuwa Mkoa umeshakamilisha maandalizi yake kwa kutoa elimu kuanzia ngazi za chini licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao wanataka kurudisha nyuma jitihada hizo kwa kukataa kuhesabaiwa huku wakiweka dodoso la kukataa kuhesabiwa mlangoni jambo ambalo halina tija katika maendeleo ya taifa.
‘Changamoto hii tumeshakutana nayo na tayari watu hao wameshikiliwa na vyombo vya dola ili uchunguzi zaidi ufanyike kwani sheria ya sense inasema mtu ambaye atapinga kwa makusudi kuhesabiwa atachukuliwa hatua kali za kisheria’’alisema Bw. Bendara.
Alisema kuwa zipo changamoto nyingine kama baadhi ya wananchi kuchapisha fulana za kukataa kuhesabiwa mpaka dodoso la dini liwepo sambamba na changamoto ya watu wenye ulemavu kuona kuwa hawajashirikishwa kikalifu katika zoezi zima la sensa.
Aliongeza kuwa ili kuhakikisha Mkoa wa morogoro unafanikiwa katika zoezi la sense ni vyema vyombo vya habari vilivyopo vikahakikisha vinatumia fursa zilizopo katika kuzidi kutoa elimu zaidi kuhusu sensa kwa njia ya Runinga ,radio na magazeti ili kila mtu aone ni wajibu wake kushiriki kikamilifu kwani hilo ni zoezi la kitaifa lenye lengo la kuleta maendeleo.
‘’Kila mwananchi atambue kuwa zoezi la sense ni kwa ajili ya maendeleo yao kwani serikali haitaweza kupanga mipango yoyote ile ya kimaendeleo endapo haitajua idadi kuu ya wananchi wake ili kuweza kujua au kutambua mahitaji ya wananchi wake.
Hata hivyo mbali na kuhamasisha waandishi wa habari kutumia kalamu zao aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini kusaidia zoezi hili kwa kutoa elimu ya umuhimu wa sense kwa waumini wake ili kuhakikisha Mkoa wa Morogoro unafanikiwa kwa asilimia 100 % zoezi hilo.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment